Kumchinja kondoo aliyeanguka au kugongwa

Swali: Wakati fulani inatokea kondoo akaanguka kutoka kwenye mlima kisha mmiliki wake akawahi kumchinja kabla ya kufa. Akimwacha, atakufa kwa hali yoyote. Je, anakuwa halali kwa uchinjaji huu?

Jibu: Akimuwahi wakati bado anaishi maisha tulivu, kichinjwa hicho ni halali kwa mujibu wa maoni sahihi. Lakini kama atamuwahi wakati yuko katika hali ya kukata roho, sio halali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 09/12/2023