Kumpiga risasi ng´ombe mwenye kukimbia

Swali: Ng´ombe amemkimbia mchinjaji, ambapo akampiga risasi mpaka akafa. Baada ya hapo akamleta machinjioni na kumuuza kana kwamba amemchinja kwa kisu. Je, inafaa kumla ng´ombe huyu?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wanyama wa mifugo hawa wana unyama, kama wanyama pori. Wakikukimbieni, basi wafanyeni namna hii.”[1]

Bi maana kupenyeza mahali kokote mwilini mwake. Inakuwa ndio kuchinjwa kwake. Kwa sababu hilo ndio liwezekanalo.

[1] al-Bukhaariy (3075).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 09/12/2023