Kukutana kwa ajili ya kumbukumbu ya maiti

Swali: Mume wake amekufa akiwa katika nyumba ya kukalia eda. Baadhi ya dada wanataka kumtembelea nyumbani kwake na kufanya ukumbusho ambapo mmoja atazungumza kuhusu dini. Je, jambo hili linakubalika kwa mujibu wa Shari´ah au halikubaliki?

Jibu: Halina msingi ikiwa wanafanya hivo kwa ajili ya kutoa rambirambi. Haitakikani ikiwa wanakuja kufanya rambirambi kwa ajili ya kifo hicho. Hata hivyo ni sawa ikiwa wanahitaji nyumba yao na wakaja kuwapikia chakula wao na wageni wao. Ni sawa ikiwa majirani wanahitaji nyumba na nyumba yao ni ndogo ambapo wakahitaji nyumba ya huyo mwanamke aliyekaa eda ambayo watawasaidia kupika chakula kwa ajili ya wageni wao. Huku ni kusaidiana.

Swali: Wanafanya ukumbusho ambapo kuna mmoja anayezungumza n.k.

Ibn Baaz: Kwa ajili ya maiti au kwa ajili ya nini?

Mwanafunzi: Kwa kweli sijui hivi ndivo wanavosema. Wanataka kujua kama maneno haya yanayozungumzwa yanakubalika kwa mujibu wa Shari´ah au hayakubaliwi?

Ibn Baaz: Hapana, hayakubaliwi kwa mujibu wa Shari´ah. Lakini hapana vibaya ikiwa mmoja katika ndugu zao amewaalika katika chakula na wakapenda kukumbushana.

Mwanafunzi: Kuhusu kitendo hichi hakifai?

Ibn Baaz: Haifai kufanya ukumbusho usiokuwa na sababu. Jaabir (Radhiya Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tulikuwa tunazingatia kukusanyika kwao na maiti na kutengeneza chakula ni katika kuomboleza.”

Lakini ikiwa kuna sababu; mtu amewaalika ndugu zake, wamefika kutoka safirini, amepona maradhi yake, anawaalika ndugu zake ambapo akawaandalia chakula hicho katika nyumba ya yule mwanamke aliyekaa eda – kwa sababu yeye nyumba yake ni ndogo – ni katika njia ya kusaidiana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23240/حكم-اقامة-جلسة-للذكرى-في-بيت-العزاء
  • Imechapishwa: 05/12/2023