03. Hadiyth “Allaah anamdhamini muumini muda wa kuwa… “

328 – ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ستُّ مجالسَ؛ المؤمن ضامنٌ على الله تعالى ما كان في شيء منها: في مسجدِ جماعةٍ، وعند مريضٍ، أو في جنازةٍ، أو في بيتِهِ ، أو عندَ إمامٍ مُقْسِطٍ يُعَزِّرُهُ ويُوَقِّرُهُ، أو في مَشهدِ جهادٍ

“Allaah (Ta´ala) anamdhamini muumini muda wa kuwa anakuwa katika moja ya vikao vita: katika msikiti wa mkusanyiko, kwa mgonjwa, katika mazishi, katika nyumba yake[1], kwa kiongozi mwadilifu anayemtukuza na kumuheshimu au katika uwanja wa jihaad.”[2]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” na al-Bazzaar kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa nzuri hivo. Hata hivyo imepokelewa kupitia kwa Mu´aadh na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[1] Bi maana anakaa nyumbani kwake kwa kuepuka kushiriki shari. Kama ilivyo katika Hadiyth ya Mu´aadh aliyoashiria mtunzi wa kitabu. Inasema:

أو قعد في بيته؛ فَسَلم، وسَلِمَ الناس منه

“… au akakaa nyumbani kwake akasalimika yeye na watu wakasalimika naye.”

[2] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/251)
  • Imechapishwa: 05/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy