13. Kushuka kwa Mola kila usiku katika mbingu ya chini ni jambo ambalo limesihi kupokelewa kwa maafikiano

Kushuka kwa Mola kila usiku katika mbingu ya chini ni jambo ambalo limesihi kupokelewa kwa maafikiano. al-Bukhaariy na Muslim wameipokea kupitia kwa Maalik bin Anas, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa al-Agharr na Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah.

Abu ´Aliy Zaahir bin Ahmad ametukhabarisha: Abu Ishaaq Ibraahiym bin ´Abdis-Swamad ametuhadithia: Abu Musw´ab ametuhadithia: Maalik ametuhadithia …:

Abu Bakr bin Zakariyyaa ametuhadithia: Abu Haatim Makkiy bin ´Abdaan ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia: Nilimsomea Ibn Naafiy´ na Mutwarrif amenihadithia, kutoka kwa Maalik…

Abu Bakr bin Zakariyyaa ametuhadithia: Abul-Qaasim ´Ubaydullaah bin Ibraahiym bin Baakuuyah amenikhabarisha: Yahyaa bin Muhammad ametuhadithia: Yahyaa bin Yahyaa ametuhadithia: Nilimsomea Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab az-Zuhriy, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr na Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka kila usiku katika mbingu ya chini ya dunia pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na anasema: “Nani anayeniomba Nimpe? Ni nani anayeniuliza Nimpe? Ni nani anayetaka nimsamehe Nimghufurie?”

Hadiyth hii imepokelewa kupitia njia nyingi kutoka kwa Abu Hurayrah.

al-Awzaa´iy ameipokea kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, ambaye amepokea kutoka kwa Abu Salamah, ambaye amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

Yaziyd bin Haaruun na maimamu wengine wameipokea kutoka kwa Muhammad bin ´Amr, ambaye ameipokea kutoka kwa Abu Salamah, ambaye ameipokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

Maalik ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy, ambaye ameipokea kutoka kwa al-A´raj, ambaye ameipokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

Maalik ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy, ambaye ameipokea kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, ambaye ameipokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

´Ubaydullaah bin ´Amr ameipokea kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqburiy, ambaye ameipokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

´Abdul-A´laa bin Abiyl-Musaawir na Bashiyr bin Sulaymaan wameipokea kutoka kwa Abu Haazim, ameipokea kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 198-206
  • Imechapishwa: 06/12/2023