Makatazo kuketi kitambo kirefu baada ya chakula?

Swali: Je, kumepokelewa makatazo ya kukaa kwa muda mrefu baada ya kumaliza kula?

Jibu: Sijafikiwa na chochote.

Swali: Vipi ikiwa mjinga anakemea kitendo hichi?

Jibu: Afunzwe. Mjinga afunzwe.

Swali: Kile chakula kilichobaki kinasamehewa [endapo kitamwagwa]?

Jibu: Kinatakiwa kushughulikiwa; ima wapewe wanyama, kuku au kizikwe kwenye udongo msafi. Hapana vibaya kikiliwa. Ikiwa meza ni safi ni sawa iwapo kitaliwa.

Swali: Asikemewe ambaye atakila?

Jibu: Hapana vibaya kikiliwa. Ni sawa pia wakipewa nacho kuku, njiwa au kikawekwa maeneo pasafi juu ya paa kwa ajili ya ndege.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23238/حكم-الجلوس-بعد-الطعام-والتصرف-ببقاياه
  • Imechapishwa: 05/12/2023