Swali: Mmoja wetu hubeba msahafu mfukoni mwake na huenda akaingia nao chooni. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kubeba msahafu mfukoni inajuzu. Haijuzu kwa mtu kuingia chooni ilihali yuko na msahafu. Auweke msahafu sehemu nzuri ili kukiadhimisha na kukiheshimu Kitabu cha Allaah. Lakini akilazimika kuingia nao kwa kuogopa usiibwe lau atauacha nje inajuzu kuingia nao kwa dharurah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/40)
  • Imechapishwa: 22/08/2020