Inafaa kumpa kafiri Qur-aan iliyotarjumiwa?

Swali: Je, tuna haki ya kumwacha mnaswara kwa lengo la kuongozwa na Allaah akasoma Qur-aan iliyotarjumiwa hata kama atakuwa hana wudhuu´?

Jibu: Kulingania katika njia ya Allaah ndio mfumo wa Mitume. Amesema (Ta´ala):

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi mimi na anayenifuata. Na Utakasifu ni wa Allaah, nami si miongoni mwa washirikina”.” (12:108)

Kumpa nuskha iliyo na tarjama ya maana ya Qur-aan tukufu ni miongoni mwa aina za kulingania katika dini ya Allaah. Ni sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/41)
  • Imechapishwa: 22/08/2020