Kutumia Aayah za Qur-aan katika mazungumzo ya kawaida

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Qur-aan wakati mmoja wetu anapofikwa na kitu katika mambo ya dini? Kwa mfano mmoja wetu kusema pale anapofikwa na matatizo au dhiki:

تَؤُزُّهُمْ أَزًّا

“Wawachochee kwa uchochezi”

Au wakati anapokutana na rafiki yake:

جِئْتَ عَلَىٰ قَدَرٍ يَا مُوسَىٰ

“Kisha ukaja [kwa miadi] ya makadirio, ee Muusa.” (20:40)

Au wakati anapotaka kula:

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ

“Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita.”? (69:24)

Na Aayah nyinginezo ambazo zinatumiwa na watu leo.

Jibu: Bora ni kuacha kutumia maneno kama hayo na mfano wake ili kuitakasa Qur-aan na kuilinda na yasiyostahiki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/56)
  • Imechapishwa: 22/08/2020