Kusoma Qur-aan kwa sauti ya juu msikitini

Swali: Je, inajuzu kusoma Suurah Yaa Siyn kwa sauti ya juu msikitini au hapana?

Jibu: Haijuzu kwa yeyote kunyanyua sauti yake kwa kusoma Qur-aan msikitini, si kwa Suurah Yaa Siyn wala Suurah nyingine, si ndani ya swalah wala nje ya swalah. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka akawakuta watu wanaswali na wanasoma kwa sauti ambapo akasoma:

“Enyi watu! Kila mmoja wenu anamnong´oneza Mola Wake. Hivyo baadhi wasisome kwa sauti ya juu kwa wengine.”

Isitoshe kufanya hivo kuna kushawishana na kuudhiana.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/24)
  • Imechapishwa: 22/08/2020