Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuna mapote na wanafalsafa wamekosea katika jina “Tawhiyd”.

Ndio, wameifasiri Tawhiyd kwa majina mbalimbali:

1 – Watu wa imani na wanachuoni wameifasiri Tawhiyd kuwa ni kumpwekesha Allaah (Ta´ala) kwa ´ibaadah na kuacha ´ibaadah ya kuabudu asiyekuwa Yeye.

2 – Watu wa shirki wamefasiri Tawhiyd kwamba ni kuabudia makaburi, makaburi yaliyojengewa. Wamefasiri na kuonelea kuwa hii ndio Tawhiyd na wanamkataza yule anayeamrisha kumuabudu Allaah peke yake na anapinga ´ibaadah ya kumuabudu asiyekuwa Yeye. Wanamkemea mtu huyu.

3 – Watu wa Wahdat-ul-Wujuud wamefasiri Tawhiyd kwamba ni kuamini kuwa ulimwengu wote huu ni Allaah na haugawanyiki. Mwenye kuugawanyisha kati ya viumbe na Muumba, huyu ni mshirikina.

4 – Mu´tazilah na Jahmiyyah wanasema kuwa Tawhiyd ni kupinga sifa. Yule mwenye kumthibitishia Allaah kuwa na majina na sifa, basi huyu ndio mshirikina na mwenye kuyapinga ndio mpwekeshaji.

Hizi ndio tafsiri zao kwa neno “Tawhiyd”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1430-4-15.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015