Allaah yuko karibu na waja wake na wakati huohuo yuko juu

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema::

“Imepokelewa ya kwamba baadhi ya Maswahabah walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee Mtume wa Allaah! Je, Mola Wetu yuko karibu tumnong´oneze au yuko mbali tunyanyua sauti zetu?” Ndipo Allaah akawa ameteremsha Aayah hii.”[1]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) yuko karibu kwa waja Wake na wakati huo huo yuko juu ya viumbe Wake. Yuko karibu kwa kusikia du´aa za waja Wake, bali anasikia siri zao na yale wanayonong´onezana, anajua mpaka yale yaliyomo ndani ya nafsi zao hata kama hawakuyatamka. Yuko karibu nao (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hii Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

“Mola wenu amesema: “Niombeni Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu, basi watauingika [Moto wa] Jahanam hali ya kuwa ni wadhalilifu.” (40:60)

[1] 02:186

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1430-2-19.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015