Mtume (´alayhis-Salaam) juu ya viongozi madhalimu

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametueleza mambo haya yote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpole na wakati huo huo ni mpambanaji ambaye hakubaliani na upotevu kamwe, lakini hivyo anatazama manufaa na madhara kwa Waislamu na analinganisha kati ya hayo mawili. Ukandamizaji wa watawala na kupinda kwao ni madhara tena makubwa, lakini pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuwa na subira juu yao bila ya kujali ni kiasi gani ufisadi wao utafikia, mpaka pale watapotoka katika Uislamu utokaji wa wazi usokuwa na mashaka na wasiwasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio mtu mwenye ghera zaidi juu ya Dini baada ya Allaah. Lakini pamoja na yote haya Ameamrisha kuwa na subira (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, tangu wakati wa Maswahabah mpaka hivi leo msimamo wao hautofautiani na hautoki katika maelekezo ya Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 07/05/2015