Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) waliona upotevu wa al-Hajjaaj [bin Yuusuf], ikiwa ni pamoja na ´Abdullaah bin ´Umar, Jaabir [bin ´Abdillaah], Abu Sa´iyd [al-Khudriy], Anas bin Maalik na mfano wa watu kama hawa. Kadhalika waliona upotevu wa Yaziyd [bin Mu´aawiyah]. Hawakuzidisha juu ya kuwaamrisha Ummah kuwa na subira. Baadhi ya watu walienda kinyume na Maswahabah na wakafanya migomo. Damu zikamwagwa na heshima zikakiukwa na kukatokea madhara yanayojua Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Lakini walijuta baada ya hapo.

Kuharamisha uasi [kwa watawala waislamu] sio ubaraka na sio ujajusi kama wanavyosema hawa Khawaarij wa leo. Kinyume chake ni kutekeleza maamrisho ya Allaah na kufuata mfumo wa Allaah na mfumo uliyoweka Mtume huyu mtukufu na maimamu wa uongoofu katika kila zama na mahala.

Wakati wa Ahmad bin Hanbal, mtawala katika zama zake alitangaza kauli ya kusema kuwa Qur-aan imeumbwa. Hii ni kufuru. Wanachuoni wakaja na kumshauri kufanya uasi, akakataa. Akasema tendo hili litawaangamiza Waislamu na kuwaletea madhara na kumwaga damu zao na kukiukwa heshima zao na kadhalika. Akakataa hilo. Je, Ahmad bin Hanbal ni kibaraka au ni jasusi? Alitiwa jela, akapewa kipigo, wakafungwa ndugu zake, wakapewa mitihani chungunzima na baadhi yao wakauawa, lakini pamoja na hayo yote akaamrisha kuwa na subira.

Huu ndio mfumo sahihi. Hata kama kutadhihiri kufuru ya wazi na katika kufanya uasi [kwa watawala kukawa] kuna madhara kwa Waislamu, hawafanya hivo. Ikiwa madhara ni makubwa kuliko manufaa hata kama ni kufuru ya wazi [haifai kufanya uasi] maadamu uasi unawadhuru Waislamu na unapelekea kumwaga damu zao na kukiukwa heshima zao, hakusababishwi uharibifu huu.

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameshikamana na mfumo huu na sio kwa sababu ya ubaraka na ujasusi na maneno ya kipuuzi kama wanavowasifia maadui wa Sunnah na maadui wa mfumo huu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 07/05/2015