Kufupisha swali kadri na inavyowezekana

Miongoni mwa adabu ambazo mwanafunzi anatakiwa kuzichunga ni muulizaji achunge ule ufinyu wa wakati wa anayejibu swali na aulize swali kwa matamshi yaliyo wazi ambayo hakuna ndani yake utatizi wala kumumunya maneno. Aidha ajitahidi kumsaidia anayejibu swali juu ya wakati wake ili masuala yawe na manufaa zaidi. Ninachokusudia kusema ni kwamba, usidhani huyu ambaye anakujibu au mwanachuoni ambaye amekuitikia simu yako uko peke yako. Huyu ambaye anamuuliza mwanachuoni anatakiwa kujua kuwa yuko na makumi ya watu kwa siku ambao wanauliza katika kila wakati. Ni lazima kuchunga jambo hili na kufanya adabu nao kwa kufupisha swali na kukubali jibu kwa kiasi cha yalivyojibiwa. Ikiwa swali liko wazi basi na jibu litakuwa wazi. Huoni namna ambavyo maswali ya Jibriyl kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni dalili ya uwazi wa maswali. Yale yaliyojengeka juu ya uwazi wa maswali na majibu huwa wazi. Kwa hivyo uwazi wa swali na uchache wa matamshi yake kwa kuhudhurisha upambanuzi wake na kujiandaa na swali kuwa wazi kabla hujauliza ni miongoni mwa adabu ambazo zinatakiwa kuchungwa.

Mara nyingi jibu haliwi wazi kwa sababu muulizaji hakulitengeneza swali lake vizuri. Endapo muulizaji angejiandaa kutengeneza vizuri swali lake kisha ndio akauliza, basi jibu lingekuwa wazi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ‘Abdil-‘Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Adab-us-Suwaal https://saleh.af.org.sa/sites/default/files/2017-11/006.mp3
  • Imechapishwa: 12/01/2023