Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

48 – Hayakuumbwa kama maneno ya viumbe.

MAELEZO

Maneno ya Allaah hayakuumbwa. Hapa wanarudiwa Jahmiyyah na Mu´tazilah ambao wanasema kuwa Qur-aan imeumbwa. Kwa sababu kwa mujibu wao ni kuwa Allaah hazungumzi. Wanamkanushia Allaah kuwa na sifa kwa sababu ya kuepukana na kufananisha wanakodai. Kwa kuwa hawakutofautisha kati ya sifa za Allaah na sifa za viumbe. Matokeo yake wakakimbia ushabihisho wanaofikiria na wakatumbukia katika ukanushaji unaosimangwa ambao ndio mbaya zaidi. Endapo wangemthibitishia Allaah yale aliyojithibitishia Mwenyewe na wakatambua kuwa kuna tofauti kati ya sifa za Muumba na sifa za viumbe, basi wangepatia na wakasalimika wao na kuwasalimisha wengine. Lakini wako upotofuni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 69
  • Imechapishwa: 12/01/2023