Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

49 – Yule mwenye kuyasikia na akadai kuwa ni maneno ya mtu basi amekufuru.

MAELEZO

Yule mwenye kusikia maneno ya Allaah na akadai kuwa ni maneno ya mtu, basi amekufuru. Kwa kuwa amekanusha maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla). Ikiwa Allaah hana maneno aliyoyateremsha kwa viumbe Wake, hoja itasimama kwao kwa kitu gani? Malengo yao ya kusema hivi ni kuivunja Shari´ah. Ikiwa hakuna maneno ya Allaah kati ya walimwengu, si Tawraat, Injiyl wala Qur-aan, maana yake ni kwamba watu wana udhuru mbele ya Allaah. Huu ndio ukafiri mkubwa na upotevu wa hali ya juu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 70
  • Imechapishwa: 12/01/2023