Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

50 – Allaah amemsema vibaya, akamtia aibu na akamtishia Moto. Amesema (Ta´ala):

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ

“Nitamwingiza kwenye [Moto wa] Saqar.”[1]

MAELEZO

Allaah (´Azza wa Jall) amemsimanga mwenye kusema hivo na akaifanya Qur-aan kuwa ni maneno ya watu, kama alivofanya al-Waliyd bin al-Mughiyrah al-Makhzuumiy. Alikuwa ni miongoni mwa makafiri wakubwa wa Makkah na walikuwa wakimwita “maua ya Makkah” kutokana na utukufu wake ndani ya mji. Pindi aliposikia Qur-aan kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipendekezwa nayo na akatambua kuwa sio katika maneno ya watu. Ndipo akaanza kuisifu Qur-aan na kusema kuwa sio mashairi, uchawi na kadhalika. Kwa mujibu wake Qur-aan ilikuwa ya kipekee. Wakati watu wake wa makafiri walimkaripia na kumtusi kwa sababu maneno yake maana yake ni kuwa ametambua ujumbe wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ndipo akabadilisha maneno na kusema:

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ

“Hii si chochote isipokuwa ni maneno ya mtu.”

Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akateremsha:

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ ثُمَّ نَظَرَ ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ

“Hakika yeye alitafakari na akakadiria, basi alaaniwe namna alivyokadiria, kisha alaaniwe namna alivyokadiria, kisha akatazama, kisha akakunja kipaji na akanuna, kisha akageuka nyuma na akafanya kiburi. Akasema: “Hii si chochote isipokuwa ni uchawi unayonukuliwa.  Hii si chochote isipokuwa ni kauli ya mtu.”[2]

Kisha Allaah (´Azza wa Jall) akasema:

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ

“Nitamwingiza kwenye [Moto wa] Saqar.”

Nayo ni Moto.

[1] 74:26

[2] 74:18-25

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 12/01/2023