Kufunga siku 1 au 2 kabla ya Ramadhaan kwa ajili ya kuchukua tahadhari

Swali: Je, inafaa kwa mtu ambaye ametia shaka kuanza kwa Ramadhaan kufunga siku moja kabla yake?

Jibu: Wako katika Hanaabilah wenye kuonelea hivo. Lakini sahihi ni kwamba asifunge. Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili.”[1]

´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Yeyote mwenye kufunga siku ya shaka, basi hakika amemuasi Abul-Qaasim.”[2]

Kwa hivyo maoni sahihi ni kwamba mtu asifunge. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Fungeni kwa kuuona na mfungue kwa kuuona. Mkifunikwa na mawingu, basi kamilisheni idadi ya Sha´baan thelathini.”[3]

Kwa hivyo hakuna kilichobaki baada ya ubainifu huu.

[1] al-Bukhaariy (1914) na Muslim (1082).

[2] al-Bukhaariy (03/27).

[3] al-Bukhaariy (1909).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 75
  • Imechapishwa: 15/03/2024