Amekula baada ya alfajiri siku ya kwanza bila kujua kuwa ni Ramadhaan

Swali: Mtu akiamka kutoka usingizini baada ya kupambazuka alfajiri siku ya kwanza ya Ramadhaan ambapo akala ilihali hajui kuwa siku hiyo ni Ramadhaan. Baadaye ndio akaelezwa. Je, anatakiwa kufunga au kula?

Jibu: Afunge na haimdhuru kwa sababu alidhani kubakia kwa usiku. Aendelee kufunga na swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 15/03/2024