Adhaana ya Fajr wakati tonge lipo mdomoni mwa mfungaji

Swali: Je, ni lazima kwa mtu anayekula daku kutema kilichomo mdomoni mwake muadhini anapoadhini au akimeze?

Jibu: Kuhusu kilichomo mdomoni mwake asikiteme. Lakini asichukue tonge lingine baada yake; isipokuwa maji. Abu Daawuud amepokea katika “as-Sunan” yake kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Akiadhini muadhini na chombo kiko mkononi mwa mmoja wenu, basi achukue kutoka humo haja yake.”

Kwa hivyo hapana vibaya akanywa akiadhini muadhini kwa sharti maji yawe tayari mkononi mwake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 76
  • Imechapishwa: 15/03/2024