Kuchukulia wepesi wanawake kufunika mikono na miguu katika swalah

Swali: Wanawake wengi wanachukulia wepesi katika swalah zao ambapo inaonekana mikono yao au sehemu yake na vivyo hivyo miguu yake. Je, kipindi hicho swalah inasihi?

Jibu: Ni lazima kwa mwanamke muungwana ambaye ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia kufunika mwili wake mzima ndani ya swalah usipokuwa uso na viganja vya mikono. Kwa sababu yeye wote ni ´awrah. Akiswali na ikaonekana sehemu ya ´awrah yake kama vile unyayo, mguu, kichwa au baadhi yake basi swalah yake haitosihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa kwa Khimaar.”

Ameipokea Ahmad na watunzi wa Sunan isipokuwa an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Makusudio ya mwenye hedhi ni yule ambaye amebaleghe.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke ni ´awrah.”

Abu Daawuud (Rahimahu Allaah) amepokea kupitia kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyesimulia kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mwanamke anayeswali kwenye shuka ya juu, Khimaar pasi na shuka ya chini akasema:

“Ikiwa shuka ya juu ni ndefu inafunika mguu mzima.”

Haafidhw Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema katika “Buluugh-ul-Maraam”:

“Maimamu wameona kuwa imesihi kutoka kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa).”

Akiwa mbele ya wanamme wa kando basi ni lazima kwake pia kufunika uso na viganja vya mikono.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/409)
  • Imechapishwa: 02/10/2021