Swali: Baadhi ya watu wanapoulizwa ni kwa nini wanachelewesha swalah ya ´Ishaa wakati wa kazi au kitu kingine wanajengea hoja kwa kusema kwamba ´Ishaa wakati wake ni mpaka kabla ya nusu ya usiku na hivyo wakati ni mpana. Tunatumai muheshimiwa utatufafanulia masuala haya na hukumu yake pamoja na kututajia dalili juu ya hilo.

Jibu: Ni lazima kwa kila muislamu kuswali ´Ishaa na nyenginezo pamoja na mkusanyiko. Haijuzu kuichelewesha na kushughulika na kazi. Kwa sababu kuitekeleza ndani ya mkusanyiko ni jambo la lazima. Haijuzu kwa yeyote kukosa mkusanyiko isipokuwa kutokana na udhuru unaokubalika katika Shari´ah kama mfano wa ugonjwa na mfano wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Akaulizwa Ibn ´Abbaas: “Ni udhuru upi?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/388)
  • Imechapishwa: 02/10/2021