Wafanyikazi makafiri wanaodhihirisha maasi katika nchi za Kiislamu

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuwakemea baadhi ya wafanyikazi wanaoingia nchini wasiokuwa waislamu wakati wanapovaa dhahabu na kuzionyesha shingoni mwao au masikioni mwao?

Jibu: Wakemewe. Ni lazima kwao kulazimiana na mila za nchi na desturi za Kiislamu. Ni kama ambavo haifai kwao kuvuta sigara au kula mchana wa Ramadhaan mbele za watu. Lakini ndani ya nyumba zao na maeneo yao ya kibinafsi inafaa kwao kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 02/10/2021