Kuanza kutoa salamu inapendeza, lakini kuitikia ni wajibu

Swali: Mtu anapotaka kuitika simu arudishe salamu au ahakikishe ni nani anayepiga simu kisha ndio aitikie salamu?

Jibu: Ikiwa ametoa salamu amuitikie salamu. Ikiwa hakutoa salamu amuulize yeye ni nani. Baada ya hapo ndio aseme:

السلام عليك

“Amani iwe juu yako.”

Swali: Kwa msemo mwingine yeye ndiye aanze kuto salamu?

Jibu: Akianza yeye ni sawa. Vinginevyo anza wewe.

Swali: Bora zaidi si yule wa mwisho?

Jibu: Yule wa mwanzo hana haki zaidi ya kuanza kuliko yule wa mwisho.

Swali: Unamaanisha nini?

Jibu: Ninachomaanisha ni kwamba yule wa kwanza hana haki zaidi ya kuanza kutoa salamu kuliko yule wa mwisho. Kwa sababu Allaah amesema:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (04:86)

Wanazuoni wamesema kwamba inapendeza kuanza kutoa salamu. Lakini ni wajibu kuitikia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23381/هل-يبدا-بالسلام-عند-الرد-على-الهاتف
  • Imechapishwa: 08/01/2024