Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mambo manne yule anayeyakusanya anakuwa ni mnafiki wa kweli na ambaye atakuwa na sifa yake moja katika mambo hayo basi atakuwa na sifa ya unafiki mpaka atakapoiacha; akiaminiwa hufanya khiyana, akisema anasema uwongo, anapoahidi anavunja ahadi yake na anapogombana hufanya uovu.”[1]

Jibu: Unafiki wa kimatendo. Huu unaitwa kuwa ni unafiki wa kimatendo. Lakini unaweza kumpelekea mtu katika unafiki wa kiitikadi. Tunamuomba Allaah usalama. Unaweza kumpelekea huko. Hata hivyo hakufuru kwa hilo. Isipokuwa ikiwa utampelekea katika ´Aqiydah  au akaona kuwa sifa hiyo ni halali.

[1] al-Bukhaariy (33) na Muslim (58).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23389/معنى-النفاق-في-حديث-اربع-من-كن-فيه
  • Imechapishwa: 21/01/2024