26. Hadiyth ”Uhai wangu ni kheri kwenu na kifo changu… “

26 – al-Hajjaaj bin al-Minhaal ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Kathiyr Abul-Fadhwl, kutoka kwa Bakr bin ´Abdillaah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

حياتي خير لكم، ووفاتي خير لكم، تحدثون فيحدث لكم، فإذا أنا مت عرضت عليَّ أعمالكم فإن رأيت خيراً حمدت الله، وإن رأيت شراً استغفرت الله لكم

”Uhai wangu ni kheri kwenu na kifo changu ni bora kwenu. Mnazungumza na mnazungumziwa. Nitapokufa, basi matendo yenu yataonyeshwa kwangu. Nikiona kheri, basi nitamuhimidi Allaah, na nikiona shari, basi nitakuombeeni msamaha kwa Allaah.”[1]

[1]  Hii ni cheni ya wapokezi nyingine ambayo ni nzuri kufika mpaka kwa Bakr bin ´Abdillaah. Wanamme wake ni wanamme wa Muslim isipokuwa Kathiyr Abul-Fadhwl. Ibn Abiy Haatim amemtaja katika “al-Jarh wat-Ta´diyl” pasi na kumjeruhi wala kumsifu. Ibn-ul-Qattwaan amesema:

“Hali yake haijulikani.”

Maneno haya yameraddiwa na Ibn Hajar katika “Lisaan-ul-Miyzaan” na akasema:

“Bali ni mwenye kujulikana.”

Kisha akarefusha katika kuyabainisha hayo. Miongoni mwa aliyoyasema ni kwamba Ibn Hibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat” na makumi ya wapokezi wamepokea kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 39
  • Imechapishwa: 08/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy