25. Hadiyth ”Uhai wangu ni kheri kwenu… “

25 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia: Ghaalib al-Qattwaan ametuhadithia, kutoka kwa Bakr bin ´Abdillaah al-Muzaniy, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

حياتي خير لكم، تحدثون ويحدث لكم، فإذا أنا مت كانت وفاتي خيراً لكم، تعرض عليَّ أعمالكم، فإن رأيت خيراً حمدت الله، وإن رأيت غير ذلك استغفرت الله لكم

”Uhai wangu ni kheri kwenu. Mnazungumza na mnazungumziwa. Nitapokufa, kifo changu kitakuwa ni kheri kwenu. Matendo yenu yataonyeshwa kwangu. Nikiona kheri, basi nitamuhimidi Allaah, na nikiona kinyume na hivo, basi nitakuombeeni msamaha kwa Allaah.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. al-Bazzaar ameipokea kwa cheni ya wapokezi yenye kuungana kupitia kwa Ibn Mas´uud. Haafidhw al-´Iraaqiy amesema:

“Wanaume wake ni wanaume wa Swahiyh, isipokuwa ´Abdul-Majuud bin Abiy Rawaad, hata kama Muslim amesimulia kutoka kwake na Ibn Ma´iyn na Nasaa´iy amemzingatia kuwa ni madhubuti, amedhoofishwa na baadhi.”

Kisha baadaye nikahakiki kosa la ´Abdul-Majiyd juu ya Hadiyth hii kutoka kwa Ibn Mas´uud na kuona kuwa ni mnyonge kutoka katika njia zote katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (979).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 08/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy