Katika hali hii ni sawa kwenda msikiti wa mbali

Swali: Vipi mtu kukusudia kwenda katika msikiti ulio mbali zaidi licha ya kuwa kuna msikiti ulio karibu?

Jibu: Ikiwa kuna manufaa ni sawa. Ikiwa kwenda kwake katika msikiti ulio mbali zaidi hakuna madhara na wala hakupelekei katika dhana mbaya ni sawa. Lakini ikiwa msikiti ulio karibu unawakusanya watu, kuna ukumbusho, mawaidha au wanamuogopa na hivyo majirani zake wanahudhuria, kwa maana nyingine ni kwamba kuna manufaa kwa yeye kuhudhuria msikiti ulio karibu.

Swali: Vipi kwa anayefata sauti nzuri?

Jibu: Haina neno. Ni kusudio jema. Kama mfano wa Tarawiyh na mfano wake kama vile Fajr. Ni kusudio jema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22518/ما-حكم-من-يتعمد-الذهاب-للمسجد-الابعد
  • Imechapishwa: 17/06/2023