Aache kuswali ikiwa anasikiliza nyimbo?

Swali: Wakati mwingine watu wa kawaida wanamuona mtu anasikiliza nyimbo na wakati huohuo anaswali ambapo wanamwambia aache kuswali muda wa kuwa anasikiliza nyimbo na kwamba ni miongoni mwa wanafiki.

Jibu: Hapana, hili ni kosa. Aswali na ahifadhi vipindi vya swalah na Allaah amwongoze. Ajiepushe na yale aliyoharamisha Allaah na swalah itamzuia kutokana na hili akiichunga. Mwishowe ataacha mambo haya:

إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ

“Hakika si vyenginevyo swalah inazuia machafu na maovu.”[1]

Yule mwenye kuihifadhi vilivyo basi itamzuia kutokana na shari.

[1] 02:03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22519/حكم-من-يقول-لمن-يسمع-الاغاني-لا-تصلي
  • Imechapishwa: 17/06/2023