“Kama humuoi msichana fulani basi toka nyumbani kwangu”

Swali: Baba yangu akinilazimisha na kunambia kwamba nisiingie nyumbani kwake kama sikumchumbia msichana fulani.

Jibu: Ikiwa mwanamke huyo hanasibiani naye basi hakumlazimu:

“Hakika si vyenginevyo utiifu unakuwa katika mema.”

Hakumlazimu kumtii isipokuwa katika mema. Akiwa ni mwenye kunasibiana naye basi anatakiwa kumtii baba yake. Akiwa hanasibiani naye, si mzuri, ubaya wa dini yake, hakumlazimu kumtii baba yake. Ndoa sio jambo jepesi. Ni jambo kubwa.

Swali: Baba yangu atanifukuza nyumbani.

Jibu: Akimuoa kwa sababu ya baba yake basi Allaah amjaze kheri.

Swali: Kwa maana nyingine afanye subira?

Jibu: Ndio, asubiri. Pengine Allaah akawakusanya:

فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا

“Pengine ikiwa mnachukia jambo na Allaah akalijaalia ndani yake kuwa na kheri nyingi.”[1]

Huenda akamuoa ilihali ni mwenye kumchukia kasha Allaah akazikutanisha nyoyo zao.

[1] 04:19

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22292/حكم-من-يلزمه-والده-بخطبة-فتاة-معينة
  • Imechapishwa: 29/01/2023