Kafara ya kumfananisha mke na mama haiwajibiki endapo mume atamwacha?

Swali: Kafara ya mume kumfananisha mke na mama yake inadondoka akimtaliki mwanamke huyo?

Jibu: Katika hali hiyo kafara ya kumfananisha mke na mama haitomuwajibikia. Isipokuwa ikiwa atamjamii. Akimtaliki atakuwa hana kafara. Lakini akimrejea haifai kumwingilia mke mpaka kwanza atoe kafara hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21962/هل-تسقط-كفارة-الظهار-بطلاق-الزوجة
  • Imechapishwa: 06/10/2022