Swali: Viatu vya ngozi ya nguruwe?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo. Salama zaidi ni kuacha kufanya hivo. Avae viatu vya ngozi ya mnyama aliye halali; ngamia, kondoo na ng´ombe. Kwa sababu kuna tofauti juu ya uhalali wa ngozi ya nguruwe inaposafishwa. Baadhi ya wanazuoni wanaiharamisha hata kama itasafishwa.

Swali: Kwa hiyo bora ni kuacha kufanya hivo?

Jibu: Salama zaidi ni kuacha kufanya hivo. Kiache kile chenye kukutia shaka na badala yake kiendee kile kisichokutia shaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21955/ما-حكم-النعل-المتخذ-من-جلد-الخنزير
  • Imechapishwa: 07/10/2022