Kuchukua viatu vya mwengine msikitini kwa aliyekosa viatu vyake

Swali: Wakati fulani katika baadhi ya misikiti kunakuwa na tofauti ya viatu. Mtu asipopata viatu vyake achukue viatu vyovyote na kwenda navyo?

Jibu: Kitu hicho hakijuzu. Akidhulumiwa naye asidhulumu. Lakini endapo viatu vyake alikuwa ameviweka maeneo maalum na sehemu hiyohiyo akaona viatu vinavyofanana na vyake, kinachoonekana ni kwamba mwenye navyo amechanganyikiwa na akachukua viatu vyake. Akipata viatu vinavyofanana na viatu vyake alivyovikosa basi kinachodhihiri ni kwamba mwenye navyo amekosea. Katika hali hiyo hapana neno akachukua hivyo vilivyoko maeneo hayo ambavyo vinafanana na vyake. Lakini kusipokuwa na kufanana kati yavyo asivichukue.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21956/حكم-اخذ-نعل-من-المسجد-لمن-فقد-نعله
  • Imechapishwa: 07/10/2022