Mke kuomba idhini katika swawm ya kulipa

Swali: Je, mwanamke analazimika kumuomba idhini mume wake wakati wa kulipa swawm?

Jibu: Hapana, analazimika kuilipa. Lakini ni sawa haja ikipelekea kuchelewesha. Vilevile mume akimuomba acheleweshe. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akichelewesha kulipa swawm ya deni.

Swali: Lakini amuombee idhini mume?

Jibu: Ni vyema swawm ya deni amuombe idhini. Kwa sababu wakati wake ni mpana. Swawm ya kulipa wakati wake ni mpana.

Swali: Wakati ukiwa mfinyu?

Jibu: Wakati ukishakuwa mfinyu basi hapo hakuna idhini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21963/هل-يلزم-المراة-استىذان-زوجها-لصوم-القضاء
  • Imechapishwa: 06/10/2022