4 – Kipengele cha nne: Kila jina la Allaah linafahamisha dhati ya Allaah, sifa iliyobeba na athari inayopelekea ikiwa jina hilo linapetuka kwenda kwengine (متعديا). Hakukamiliki kuamini jina isipokuwa kwa kuthibitisha mambo yote hayo.

Mfano wa jina ambalo si lenye kupetuka kwenda kwengine ni Aliyetukuka (العظيم). Hakutimii kuliamini mpaka mtu aamini kulithibitisha kama jina moja wapo miongoni mwa majina ya Allaah linalojulisha dhati ya Allaah (Ta´ala) na sifa iliyobebwa nalo ambayo ni utukufu.

Mfano wa jina linalopetuka kwenda kwengine ni Mwingi wa huruma (الرحمن). Hakutimii kuliamini mpaka mtu aamini kulithibitisha kama jina moja wapo miongoni mwa majina ya Allaah linalojulisha dhati ya Allaah (Ta´ala), sifa iliyobeba ya rehema na ile athari inayopelekea ambayo ni kumuhurumia amtakaye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 23
  • Imechapishwa: 06/10/2022