Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Malaika huziweka mbawa zao juu ya mwenye kutafuta elimukwa kuridhia anachokifanya.”

Hii ni faida kubwa inayoonyesha fadhilah za kujifunza elimu. Makusudio hapa ni elimu ya dini, bi maana elimu aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusu elimu ya kidunia ni kwa dunia. Kutafuta elimu aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio ambayo kumekuja juu yake kusifiwa, matapo, kuhimizwa ndani ya Qur-aan na Sunnah. Elimu hii ni aina miongoni mwa Jihaad katika njia ya Allaah. Kwa sababu dini hii imesimama juu ya mambo mawili:

1 – Elimu na ubainifu.

2 – Silaha ya upanga na mikuki.

Mpaka baadhi ya wanachuoni wamefikia kusema ya kwamba kutafuta elimu ni bora zaidi kuliko kupigana Jihaad katika njia ya Allaah kwa silaha. Kwa sababu Shari´ah inahifadhiwa kwa elimu. Jihaad  katika njia ya Allaah kwa silaha ni jambo limejengwa juu ya elimu. Mujaahid hawezi kupigana, hawezi kugawa ngawira na wala hawezi kuhukumu kifungu isipokuwa kwa njia ya elimu. Elimu ndio mama wa kila kitu. Kwa ajili hii ndio maana Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ 

“Allaah atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mjuzi wa ndani kabisa.” (58:11)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/108)
  • Imechapishwa: 08/02/2023