Swali: Je, inatosha kafara moja kama mtu aliweka nadhiri mara nyingi?
Jibu: Ikiwa ni kwa kitendo kimoja basi atatoa kafara ya kiapo kimoja. Kwa mfano aliapa kwa jina la Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani na kila alipomuona akayakariri maneno haya mara nyingi, atatoa kafara moja. Lakini kama alikariri kwa kuapa kwa Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani, akaapa kwa Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani mwingine, akaapa kwa Allaah kwamba hatosafiri, kila kiapo katika hali hii kina hukumu moja na kafara yake ya kiapo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22715/هل-تكفي-كفارة-واحدة-اذا-تكرر-النذر
- Imechapishwa: 01/08/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Viapo vingi juu ya vitu tofauti
Swali: Kuna mtu leo amekula kiapo, kesho akala kiapo, kesho yake akala kiapo. Je, kafara moja inatosha? Jibu: Ikiwa ni juu ya kitu kimoja. Swali: Viapo vya kutofautiana? Jibu: Unafahamu au hufahamu? Kwa mfano mtu anaapa hii leo kwamba hatomzungumzisha fulani, kesho akaapa kwamba hatomzungumzisha mtu mwingine ambaye anaitwa Zayd,…
In "Nadhiri, yamini na kafara mbalimbali"
Namna ya kukafiria kafara nyingi
Swali: Mtu ambaye ana kafara nyingi za kiapo anakafiria kwa kila kiapo kimoja au inatosha kwake kuwalisha masikini kumi mara moja? Jibu: Inategemea. Ikiwa kiapo kimekariri na kimetolewa kwa mara moja basi atakafiria kafara moja. Ama ikiwa ni viapo vingi basi itabidi atoe kafara nyingi. Kwa mfano akiapa kwa Allaah…
In "Nadhiri, yamini na kafara mbalimbali"
Je, kiapo kizito kina kafara?
Swali: Je, kiapo kizito (اليمين الغموس) kina kafara? Jibu: Hakina kafara. Hata hivyo dhambi yake ni kubwa. Kafara inakuwa katika mambo mepesi ya masiku yajayo ambayo ameapa kwamba hatoyafanya kisha akayafanya, mambo ambayo ameapa kwamba atayaacha kisha akayafanya au kwamba hatoyafanya kisha akayafanya. Kuhusu kiapo kizito ni khatari. Mtu akifanya…
In "Nadhiri, yamini na kafara mbalimbali"