Je, inatosha kafara moja kama mtu aliweka nadhiri mara nyingi?

Swali: Je, inatosha kafara moja kama mtu aliweka nadhiri mara nyingi?

Jibu: Ikiwa ni kwa kitendo kimoja basi atatoa kafara ya kiapo kimoja. Kwa mfano aliapa kwa jina la Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani na kila alipomuona akayakariri maneno haya mara nyingi, atatoa kafara moja. Lakini kama alikariri kwa kuapa kwa Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani, akaapa kwa Allaah kwamba hatomzungumzisha fulani mwingine, akaapa kwa Allaah kwamba hatosafiri, kila kiapo katika hali hii kina hukumu moja na kafara yake ya kiapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22715/هل-تكفي-كفارة-واحدة-اذا-تكرر-النذر
  • Imechapishwa: 01/08/2023