Kinachompasa aliyeweka nadhiri ya maasi

Swali: Ni ipi hukumu ya nadhiri ya maasi?

Jibu: Atoe kafara ya kiapo. Nadhiri iliyoibahishwa na nadhiri inayochukiza zote zinatolewa kafara ya kiapo. Kuhusu nadhiri ya utiifu ni lazima kuitekeleza. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Aliyetia nadhiri ya kumtii Allaah, basi amtii, na aliyetia nadhiri ya kumuasi Allaah, basi asimuasi.”

Nadhiri ya ´Aaishah inazungukia baina ya nadhiri inayochukiza na nadhiri ya maasi. Kwa sababu ni nadhiri ya kukata kizazi na kuwasusa. Hakukingwa na kukosea. Kutokana na ukali wa ghadhabu zake aliweka nadhiri hii. Inatosha kwake kutoa kafara ya kiapo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22714/ما-حكم-الكفارة-لنذر-المعصية
  • Imechapishwa: 01/08/2023