Je, bora sujuud mbili za kusahau ziwe kabla au baada ya salamu?

Swali: Je, bora sujuud mbili za kusahau ziwe kabla au baada ya salamu?

Jibu: Inategemea. Ikiwa ni kwa kupunguza kitu inakuwa baada ya salamu.

Swali: Baadhi yao wanasujudu kabla ya salamu?

Jibu: Inasihi kabla na baada ya salamu.

Swali: Bora ni vipi?

Jibu: Ikiwa ni kwa kupunguza kitu inakuwa baada ya salamu. Kwa mfano ikiwa ametoa salamu baada ya Rak´ah tatu kisha akakumbushwa na baadaye akakamilisha, basi sujuud inakuwa baada ya salamu. Au hali inayofanana na hiyo; kwa mfano amemaliza swalah kwa kusahau kabla ya swalah kumalizika, katika hali hii atasujudu baada ya kutoa salamu. Lakini ikiwa amesahau ndani ya swalah basi katika hali hiyo atasujudu kabla ya kutoa salamu. Kwa mfano akiacha Tashahhud ya kwanza, mfano mwingine ametia shaka kama ameswali Rak´ah tatu au Rak´ah nne ambapo wakamkumbusha na baadaye akakamilisha, katika hali hii sujuud inakuwa kabla ya kutoa salamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23234/موضع-سجود-السهو-قبل-السلام-وبعده1
  • Imechapishwa: 04/12/2023