al-Haakim Abu ´Abdillaah al-Haafidhw ametukhabarisha: Abu Bakr Muhammad bin Daawuud az-Zaahid ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan as-Saamiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Muhammad bin Shabuuyah al-Marwaziy amenikhabarisha: Nimemsikia ´Aliy bin al-Husayn bin Shaqiyq akisema: Nimemsikia ´Abdullaah bin al-Mubaarak akisema:

”Tunamtambua Mola wetu kuwa juu ya mbingu saba na kwamba amelingana juu ya ´Arshi. Ametengana na viumbe Wake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah, ya kwamba Yuko hapa” na akaashiria ardhini.”

Nimemsikia al-Haakim Abu ´Abdillaah akisema katika kitabu chake ”at-Taariykh”, ambacho alikitunga kwa ajili ya wakazi wa Naysaabuur, na pia katika kitabu chake ”Ma´rifat-ul-Hadiyth” – vitabu viwili ambavyo hakuna mfano wake: Nimemsikia Abu Ja´far Muhammad bin Swaalih bin Haani’ akisema: Nimemsikia Abu Bakr Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah akisema:

”Yule asiyemtambua Allaah (´Azza wa Jall) kuwa juu ya ´Arshi Yake na kwamba amelingana juu ya mbingu Zake saba, basi amemkufuru Mola wake. Damu yake ni halali kumwagwa. Anatakiwa kutakwa kutubia na vinginevyo ikatwe shingo yake[1].  Baada ya hapo atatupwa kwenye takataka ili waislamu na wale makafiri wenye mkataba wa amani na wao wasikereke na harufu mbaya ya mzoga wake. Mali yake itakuwa fai. Si ruhusa kwa muislamu yeyote kuirithi kwa sababu muislamu hamrithi kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu.”

Imamu wetu Abu ´Abdillaah Muhammad bin Idriys ash-Shaafiy´iy (Rahimahu Allaah) amesema ndani ya kitabu chake[2] alichozungumza kwa upana juu ya suala la kumwacha huru mtumwa wa kiislamu katika kafara:

”Kutokana na Hadiyth ya Mu´aawiyah bin al-Hakam haijuzu kulipa kafara kwa mtumwa asiyekuwa muumini. Alitaka kumwacha huru kijakazi mweusi na akamuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kumwacha huru. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa mtihani na kumuuliza: ”Mimi ni nani?” Akamwashiria yeye na mbinguni.” Bi maana, wewe ni Mtume wa Allaah ambaye yuko juu ya mbingu. Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”[3]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamthibitishia Uislamu na imani yake wakati alipotambua kuwa Mola wake yuko juu ya mbingu na akamtambua kwa sifa ya kuwa na ujuu na kuwa juu. ash-Shaafi´iy amejengea hoja Hadiyth hii dhidi ya wale wanaojuzisha kumwacha mtumwa huru kafiri katika kafara, kwa sababu ya kuamini kwake ya kwamba Allaah (Subhaanah) yuko juu ya viumbe Wake, juu ya mbingu Zake saba na juu ya ´Arshi Yake. Hivo ndivo waislamu, Ahl-us-Sunnah wal-Jama´ah, daima walivyoitakidi. Yeye (Rahimahu Allaah) hakuwahi kusimulia Hadiyth Swahiyh kisha eti asionelei hivo. al-Haakim Abu ´Abdillaah (Rahimahu Allaah) ametukhabarisha: Imaam Abul-Waliyd Hassaan bin Muhammad al-Faqiyh ametukhabarisha: Ibraahiym bin Mahmuud ametuhadithia: Nimemsikia ar-Rabiy´ bin Sulaymaan akisema: Nimemsikia ash-Shaafi´iy akisema:

”Mkinisikia nasema kitu na wakati huohuo kumesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinyume chake, basi tambueni kuwa akili yangu imeniondoka.”

al-Haakim (Rahimahu Allaah) amesema: Nimemsikia Abul-Waliyd mara nyingi akisema:

”Nimehadithiwa kutoka kwa az-Za´faraaniy ya kwamba siku moja ash-Shaafi´iy alitajiwa Hadiyth ambapo bwana mmoja akauliza: ”Ee Abu ´Abdillaah! Je, wewe unaonelea hivo?” Akajibu: ”Je, waniona kwenye sinagogi au kanisa? Je, waniona na nguo za makafiri? Waniona kwenye msikiti wa waislamu, nikiwa na mavazi ya waislamu, nimeelekea Qiblah chao. Je, nisimulie Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha nisionelee hivo?”

[1] Zayd al-Madkhaliy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Si haki ya kila mmoja kusimamisha adhabu za Kishari´ah. Isipokuwa yule aliyetawalia madaraka ya waislamu. Mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye haki ya kusimamisha adhabu kama vile ya kumuua anayeua makusudi, anakata mkono wa mwizi, anampiga bakora mzinzi ambaye hajawahi kuingia ndani ya ndoa, atampiga mawe mzinzi ambaye kishawahi kuingia ndani ya ndoa na atampiga mijeledi mtu ambaye anawatuhumu wengine machafu na mnywaji pombe. Wakati mwingine adhabu inaweza kuwa kwa njia ya kuua. Yote haya ni mambo yanayopasa mamlaka. Hakuna mwengine yeyote, hata kama ni mwanachuoni,  anayo haki ya kusimamisha adhabu si juu ya nafsi yake mwenyewe wala waja wengine isipokuwa ikiwa kama ana idhini kutoka kwa mtawala, kwa mfano mahakimu wa kidini na maafisa wa polisi. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya jambo hili.” (at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 17-18)

[2] ´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy amesema:

”Bi maana kwenye kitabu chake ”al-Umm”.” (Sharh ´Aqiydat-is-Salaf wa Aswhab-il-Hadiyth, uk. 99)

[3] Muslim (537), Abu Daawuud (930), an-Nasaa’iy (3/13), Maalik (2/776), Ibn Abiy ´Aaswim (479), al-Bayhaqiy, uk. 422, Ahmad (5/447), Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1105) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 121.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 185-189
  • Imechapishwa: 04/12/2023