Abul-Hasan ´Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym bin Muhammad bin Yahyaa al-Muzakkiy ametukhabarisha: Muhammad bin Daawuud bin Sulaymaan amenihadithia: ´Aliy bin Muhammad bin ´Ubayd Abul-Hasan amenikhabarisha: Abu Yahyaa bin Bishr al-Warraaq ametuhadithia: Muhammad bin al-Ashras al-Warraaq Abu Kinaanah ametuhadithia: Abul-Mughiyrah al-Hanafiy ametuhadithia: Qurrah bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa mama yake, kutoka kwa Umm Salamah aliyesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

”Kulingana si kitu kisichojulikana. Namna haieleweki. Ni wajibu kuamini hilo na ni kufuru kukanusha jambo hilo.”[2]

Abul-Hasan bin Ishaaq al-Madaniy ametuhadithia: Ahmad bin al-Khadhir Abul-Hasan ash-Shaafi´iy ametuhadithia: Shaadhaan ametuhadithia: Ibn Makhlad bin Yaziyd al-Qahastaaniy ametuhadithia: Ja´far bin Maymuun ametuhadithia:

”Maalik bin Anas aliulizwa kuhusu maneno Yake:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

na namna Alivyolingana. Akajibu: Kulingana si kitu kisichojulikana. Namna haieleweki. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuuliza juu ya jambo hilo. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mpotevu.” Akaamrisha atolewe nje ya kikao chake.”

Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Muslim al-Isfaraayiyniy ametuhadithia: Abul-Husayn ´Aliy bin al-Hasan ametuhadithia: Salamah bin Shabiyb ametuhadithia: Mahdiy bin Ja´far bin Maymuun ar-Ramliy ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin ´Abdillaah:

”Bwana mmoja alikuja kwa Maalik bin Anas akasema: ”Ee Abu ´Abdillaah:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

Amelingana vipi?”

Sijapatapo kumuona Maalik akichukulia vibaya kabisa kama mara hiyo. Akaanza kutokwa na jasho na huku watu wanasubiri wasikie atachosema. Kisha akajivuta na kusema:

”Namna si kitu kisichojulikana. Kulingana haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo. Nachelea ukawa mpotevu.”

Kisha akaamrisha atolewe nje.”

Abu ´Aliy al-Husayn bin al-Fadhwl al-Bajaliy aliulizwa ni vipi Allaah amelingana juu ya ´Arshi ambapo akajibu:

”Sijui khabari zilizofichikana isipokuwa kile kiasi tulichofichuliwa. Yeye (´Azza wa Jall) ametueleza kuwa amelingana juu ya ´Arshi pasi na kutueleza namna Alivyolingana juu.”

[1] 20:05

[2] Ibn Taymiyyah amesema:

”Haya yamepokelewa kutoka kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa), kutoka kwake yeye na kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo cheni yake ya wapokezi sio kitu ambacho mtu anaweza kukitegemea.” (Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 34)

[3] 20:05

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 177-185
  • Imechapishwa: 04/12/2023