Makatazo ya kula matonge mawili kwa mpigo

Swali: Je, imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kula tende mbili kwa mpigo?

Jibu: Ikiwa anakula pamoja na mwingine. Isipokuwa mtu huyo akupe idhini. Ikiwa anakula pamoja na mwingine basi asifanye hivo isipokuwa kwa idhini yake. Lakini ikiwa anakula peke yake inafaa kwake kula tende mbili au tende tatu. Hapana vibaya. Ikiwa anakula na wenzake asiambatanishe; asile tende mbili, komamanga mbili wala matunda mawili. Kwa msemo mwingine aombe idhini kama anataka kuambatanisha.

Swali: Vipi ikiwa chakula ni kingi?

Jibu: Haijalishi kitu. Kama anakula na wenzake basi asiambatanishe isipokuwa kwa idhini yao.

Swali: Ni lazima apate ruhusa kutoka kwa wenzake?

Jibu: Ndio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23237/حكم-اكل-التمرتين-في-لقمة-واحدة
  • Imechapishwa: 04/12/2023