02. Hadiyth “Mtu hatolazimiana na misikiti…. “

327 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ما تَوَطّنَ رجلٌ المساجدَ للصلاةِ والذكْرِ إلا تَبَشْبَشَ الله تعالى إليه كما يَتَبَشْبَشُ أهلُ الغائب بغائبهم إذا قَدِمَ عليهم

“Mtu hatolazimiana na misikiti kwa lengo la swalah na dhikr, isipokuwa Allaah humfurahikia kama jinsi familia ya aliyeko mbali wanavyomfurahikia wakati anapowafikia.”

Ameipokea Ibn Abiy Shaybah, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh”, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim ambaye amesema:

“Ni Swahiyh kwa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

Kwa Ibn Khuzaymah imekuja:

ما مِنْ رَجلٍ كان تَوَطّن المساجدَ، فَشَغَلَهُ أمرٌ أو علةٌ ثم عادَ إلى ما كان؛ إلا يَتَبَشْبَشُ الله إليهِ كما يَتَبَشْبَشُ أهل الغائب بغائبهم إذا قدِمَ

“Hakuna mwanaume ambaye atalazimiana na misikiti ambapo akashughulishwa na jambo kisha baadaye akarudi aliyokuwemo, isipokuwa Allaah humfurahikia kama jinsi familia ya aliyeko mbali wanavyomfurahikia wakati anapowafikia.”[1]

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/251)
  • Imechapishwa: 04/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy