Swali: Inazingatiwa kuwa ni usengenyaji kumsema mtoto kwa kitu ambacho akikisikia kitamuudhi?

Jibu: Usengenaji haijuzu, sawa ikiwa ni kwa mtoto au mtu mkubwa. Kuwasema watu vibaya haijuzu. Haijalishi kitu ikiwa ni mtoto au mtu mkubwa. Mtoto ndio hana haki? Mtoto ana haki zaidi ya kutofanyiwa hivi kwa kuwa ni kiumbe dhaifu. Kwa hivyo ana haki zaidi ya kufanyiwa upole na kuonewa huruma. Alelewe vizuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020