Inajuzu kukaa kwa kuweka mguu juu ya mwingine?

Swali: Je, inajuzu kwa mtu kukaa kwa kushegama na huku amepandisha mguu juu ya mwingine au mkao huu haujuzu kutokana na yaliyopokelewa katika Hadiyth ya kwamba hii ni sifa ya Allaah (Jalla Jalaaluh) na haijuzu kwa yeyote kusifika nayo?

Jibu: Allaah anaweka mguu juu ya mwingine? Ni nani aliyesema hivi? Haina neno akakaa na huku ameweka mguu juu ya mwingine na kwa staili anayotaka. Ni nani anayezuia hili. Lililo la wajibu ni yeye kusitiri viungo vyake visivyotakiwa kuonekana. Ama staili ya kukaa akae staili yoyote ambayo ni sahali kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (60) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-28.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020