Baada ya kuingia katika swalah amekumbuka hajaswali ya kabla yake

Swali: Mtu akiingia kwenye swalah ya faradhi kisha akakumbuka kuwa hakuswali swalah ya faradhi ya kabla yake. Je, akamilishe swalah aliyonuia hivi sasa na atapomaliza aswali iliyompita?

Jibu: Ainuie ya sunnah. Anuie aliyomo kuwa ya sunnah na aikamilishe. Kisha atapotoa salamu aswali iliyompita. Halafu baada ya hapo aswali swalah ya wakati huo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (60) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-28.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020