Kukata swalah kwa ajili ya kuitikia muadhini

Swali: Muadhini aliadhini adhaana ya kwanza siku ya Ijumaa na mimi nilikuwa naswali Naafilah. Je, nikate swalah yangu kwa ajili ya kumfuata muadhini?

Jibu: Hapana, ukishaingia katika swalah usiikate:

وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ

“Wala msibatilishe matendo yenu.” (47:33)

Usikate swalah kwa ajili ya kumuitikia muadhini. Swalah imekokotezwa zaidi kwako kuliko kumfuata muadhini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (60) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-28.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020