Swali: Ni yapi makusudio ya “kwa ufahamu wa Salaf juu ya maandiko”?

Jibu: Ni jambo liko wazi. Salaf (Rahimahumu Allaah) waliyafahamu maandiko vile alivyotaka Allaah na Mtume Wake. Waliyafahamu vile yalivokuja katika Qur-aan; tafsiri ya Qur-aan Aayah hizi kuzifasiri zingine, yaliyothibiti katika Sunnah katika kuifasiri Qur-aan au yaliyothibiti katika tafsiri ya Maswahabah. Ufahamu wa Salaf umejengwa juu ya misingi hii. Huu ndio ufahamu wa Salaf. Umejengwa juu ya misingi hii. Ufahamu wao haukujengwa juu ya fikira, kama wanavyosema wafikiriaji. Umejenjwa juu ya misingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-03-11.MP3
  • Imechapishwa: 21/08/2020